1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Maelfu waandamana Israel dhidi ya mageuzi ya Mahakama

13 Februari 2023

Maelfu ya Waisraeli wameandamana leo nje ya bunge dhidi ya mageuzi tete ya mahakama yanayopangwa na serikali, ambayo yanalenga kuwapa wabunge udhibiti zaidi wa mahakama ya Juu.

https://p.dw.com/p/4NQcS
Israel Tel Aviv | Proteste gegen die Regierung
Picha: Gili Yaari/NurPhoto/picture alliance

Mageuzi hayo yaliyokaribia kuidhinishwa kupitia mfululizo wa kura bungeni, yamechochea ukosoaji mkubwa kwamba yatalipa bunge mamlaka yasiyoweza kudhibitiwa.

Wakiwa wamebeba vijibendera vya Israel, maelfu ya waandamanaji hao walibeba mabango yenye ujumbe usema, iokoe demokrasia ya Israel na kwamba ulimwengu mzima unatizama.

Katika hotuba ya nadra kwa taifa usiku wa kuamkia leo, rais wa Israel Isaac Herzog aliangazia mpango wa mageuzi huku akitahadharisha kuwa Israel iko katika hatari ya kuporomoka kisheria na kijamii.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo  Benjamin Netanyahu na washirika wake wanasema mageuzi ni muhimu kurekebisha ukosefu wa usawa wa mamlaka kati ya wawakilishi waliochaguliwa na mahakama ya juu zaidi nchini humo.