1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Hungary kuhusu kashfa ya unyanyasaji

Sylvia Mwehozi
17 Februari 2024

Maelfu ya watu waliandamana jana katika mji mkuu wa Hungary wa Budapest kupinga msamaha wa rais katika kesi ya unyanyasaji kingono watoto ambayo imekuwa mwiba wa kisiasa kwa waziri mkuu Viktor Orban.

https://p.dw.com/p/4cVkN
Hungary
Maelfu ya watu wakiandamana katika mji mkuu wa Hungary wa BudapestPicha: Denes Erdos/AP Photo/picture alliance

Maelfu ya watu waliandamana jana katika mji mkuu wa Hungary wa Budapest kupinga msamaha wa rais katika kesi ya unyanyasaji kingono watoto ambayo imekuwa mwiba wa kisiasa kwa waziri mkuu Viktor Orban. Orban hajazungumzia kashfa hiyo, lakini anatarajiwa kutoa hotuba yake ya kila mwaka ya hali ya taifa siku ya Jumamosi.

Kujiuzulu kwa Rais wa Hungary K. Novak

Mnamo Jumamosi iliyopita, rais wa Hungary na waziri wa zamani wa sheria Judit Varga, walijiuzulu baada ya kuunga mkono uamuzi wa kutoa msamaha kwa mwanamume aliyehusishwa na kashfa ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto mwaka 2023.

Kiongozi mwingine mkubwa wa kanisa la Kiprotestanti Askofu Zoltan Balog alitangaza kujiuzulu jana kuhusiana na kashfa hiyo. Askofu huyo aliwahi kuhudumu kama waziri wa serikali kipindi cha nyuma.