1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID:Uchunguzi wa mauaji ya wahamiaji watano haramu wa kiafrika

30 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEWE

Uhispania imeahidi kuanzisha uchunguzi juu ya mauaji ya watu watano waliokuwa wakijaribu kuhamia kiharamu nchini humo.

Baada ya maiti hizo kufanyiwa upasuaji ilibainika kwamba wawili kati yao waliuwawa kwa kupigwa risasi.

Wakati huo huo serikali ya Uhispania imewapeleka wanajeshi kwenye eneo hilo ili kuwasaidia polisi kushika doria.

Maafisa wa Uhispania wameeleza kwamba wawili kati ya watu watano waliouwawa walipatikana nchini Uhispani lakini wengine watatu miili yao ilipatikana Morocco.

Katika wiki za hivi karibuni maelfu ya waafrika wamekuwa wakijaribu kuingia ulaya kupitia pwani ya kaskazini mwa Morroco na hatimaye Uhispania.