1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID.Sarkozy apendekeza masharti sawa ya umoja wa ulaya dhidi ya wahamiaji wasio halali

30 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD7a

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amependekeza hatua ya pamoja ya nchi za umoja wa ulaya juu ya kuwepo masharti sawa katika sera za uhamiaji.

Sarkozy amependekeza kuwepo marufuku katika sheria ya kuwapa hifadhi wahamiaji wasio halali.

Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Ufaransa amesema katika mkutano mjini Mardrid, Uhispania kuwa hatua ya nchi moja ya ulaya ya kuwapa hifadhi wahamiaji wengi imedhuru nchi zote za umoja wa ulaya.

Nae waziri mkuu wa Uhispania Jose Luis Rodriguez Zapatero ambae mwaka jana aliidhinisha kuhalalishwa nusu milioni ya wahamiaji wasio na nyaraka nchini mwake alitetea hatua yake hiyo na kuongeza kuwa hakuhitaji mafunzo kutoka Ufaransa.

Mkutano huo umeitishwa baada ya kuingia katika visiwa vya Canary nchini Uhispania wahamiaji alfu 23 kutoka bara la Afrika katika mwaka huu pekee.