1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid wawanyatia mahasimu wao Atletico

22 Februari 2021

Real Madrid wameupunguza mwanya baina yao na vinara Atletico Madrid hadi kufikia pointi tatu baada ya Atletico kuteleza Jumamosi walipozabwa 2-0 na Levante

https://p.dw.com/p/3phuN
UEFA Champions League | Real Madrid - Manchester City | Benzema & Zidane
Picha: Reuters/J. Medina

Atletico walikuwa nyumbani kwao Wanda Metropolitano na Madrid wakashinda moja bila dhidi ya Real Valladolid.

Barcelona walitetereka Jumapili baada ya kuzuiwa sare ya bao moja na Cadiz. Huyu hapa kocha wao Ronald Koeman.

"Bila shaka nimevunjwa moyo, nimevunjwa moyo sana zaidi ya kushindwa kwetu katikati ya wiki kwasababu leo tulikwua na nafasi ya kuupunguza mwanya, hasa nyumbani, mahali ambapo tunastahili kushinda. Ni mechi ambayo hatukushuhudia matatizo mengi na ni mechi ambayo hii timu inastahili kushinda kutokana na ubora tulio nao kikosini," alisema Koeman.

Mechi ijayo, Real Madrid watakuwa wanacheza na Real Sociedad huku Atletico Madrid wakiwa na kazi ngumu dhidi ya Villareal na mashabiki wa Barcelona washikilie pumzi klabu yao itakapocheza na Sevilla ambayo inawahemea kooni katika nafasi ya nne kwenye jedwali la ligi hiyo.