1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswidi

Madege ya kivita ya Marekani yatua nchini Sweden

21 Juni 2023

Madege ya kivita ya Marekani yametuwa nchini Sweden kwa mara ya kwanza katika historia ya sasa, kutumika kwenye mazoezi ya kijeshi yatakayofanywa kwa mwaliko wa jumuiya ya kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4StfU
Deutschland, Niedersachsen, Wunstorf | Luftwaffen-Manöver Air Defender 2023
Picha: Ronny Hartmann/AFP

Madege mawili ya Marekani chapa Lancers B-IB, yalituwa katika uwanja wa ndege wa Lulea-Kallax kaskazini mwa Sweden mnamo siku ya Jumatatu kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa leo na jeshi.

Sweden yasema ni muhimu kuwa na mashirika imara

Msemaji wa jeshi la Sweden,Louise Levin ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wataendesha mazowezi hayo kwa pamoja na kikosi cha wanaanga pamoja na jeshi la nchi kavu pamoja na kikosi maalum chenye uwezo wa kutumia madege hayo. Hata hivyo haikuelezwa ni kwa muda gani mazowezi hayo yataendelea. Sweden imesema katika wakati huu uliojaa mashaka, na wakati ikisubiri kujiunga na Jumuiya ya NATO ni muhimu kuwa na washirika imara.