1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Utawala wa sheriaIsrael

Madaktari wagoma Israel kupinga mageuzi ya sheria tata

25 Julai 2023

Maelfu ya madaktari nchini Israel wamegoma hii leo, huku viongozi wa vyama vya wafanyakazi wakitishia mgomo wa nchi nzima na majaji waandamamizi wakirejea haraka kutoka ziara za nje .

https://p.dw.com/p/4UO4L
Israel | Justizreform | Protest
Picha: Corinna Kern/REUTERS

Hayo yanafanyika ikiwa ni siku moja baada ya bunge kuidhinisha sheria inayodhoofisha mamlaka ya mahakama ya juu ya nchi hiyo, ambayo wakosoaji wanasema itaondoa mfumo wa mgawanyo wa madaraka.

Muswada wa sheria hiyo ulipita katika bunge la Knesset baada ya wabunge wa upinzani kususia, huku baadhi wakimtuhumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuipeleka nchi hiyo kwenye utawala wa kiimla.

 Soma pia:Bunge la Israel lapitisha sheria tata ya mageuzi ya mahakama
Matangazo ya wino mweusi yalipamba kurasa za mbele za magazeti manne maarufu nchini Israel leo, huku waandamanaji wakiapa kuendelea kupambana dhidi ya hatua ya serikali ya mrengo mkali wa kulia ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu, kuridhia sehemu ya kwanza ya mageuzi ya mahakama ambayo wakosoaji wanahofia kuhatarisha uhuru wa mahakama.

Sheria hiyo inayoizuia mapitio ya Mahakama ya Juu kuhusu baadhi ya maamuzi ya serikali ilipitishwa katika bunge la Knesset mnamo jana Jumatatu, baada ya wabunge wa upinzani kutoka nje.

Baadhi ya watu wanamshutumu Waziri Mkuu wa muda mrefu Benjamin Netanyahu kuisukuma Israel kuelekea kwenye utawala wa kiimla.

Maandamano yaendelea kufukuta

Huku maandamano yakiigubika Israel kwa miezi kadhaa, maelfu waliingia barabarani na kukabiliana na polisi Jumatatu usiku.

Israel | Justizreform | Protest
waandamanaji wakiwa na bendera za IsraelPicha: Ronen Zvulun/REUTERS

 "Siku nyeusi kwa Demokrasia ya Israel," lilisema tangazo lililochapishwa kwenye kurasa za mbele za magazeti makubwa manne, lililolipiwa na kundi linalojieleza kuwa wafanyakazi wa teknolojia ya kiasa wenye wasiwasi.

Kura hiyo ambayo ndiyo ya kwanza katika mkururo wa hatua zinazounda mageuzi tata ya waziri mkuu Netanyahu ya mfumo wa mahakama, ilivutia nadhari kote nchini humo, ikipita licha ya miezi saba ya upinzani mkali wa umma, ahadi ya Netanyahu ya  muafaka na onyo lisilo la kawaida kutoka mshirika wa karibu zaidi wa Israel, Marekani.

Soma pia:Hotuba ya Netanyahu yaibua maandamano mapya Israel

Mmiliki wa kampuni inayoendesha maduka kadhaa mjini Jerusalem aliejitambulisha kwa jina la Boaz alifananisha kupitishwa kwa sheria hiyo kama siku za giza kwa taifa hilo la Mashariki ya Katio.

"Nadhani nchi ambayo tunaijua na kuipenda imebadilika na kuwa mbaya zaidi."

Aliongeza kuwa anayo matumaini kwamba taifa lake litarejea katika hali ya kawaida.

 Kura hiyo ilikuja saa chache baada ya Netanyahu kuruhusiwa kutoka hospitalini, ambako alikuwa amepandikizwa kidhibiti cha moyo, na kuongeza hali nyingine ya kutatanisha katika mfululizo wa matukio ambayo tayari yalikuwa ya makubwa.

Mgomo wa wafanyakazi Israel unatuma ujumbe gani?

Chama cha Madaktari wa Israeli, kinachowakilisha karibu madaktari wote wa nchi hiyo, kilitangaza kuwa watagoma kwa wingi leo kote nchini, na kushughulikia tu operesheni za dharura na kutoa huduma kwa wagonjwa mahututi.

Israel | Justizreform | Protest
Baadhi ya waandamanaji wakiwa wamevalia mavazi ya majajiPicha: Maya Alleruzzo/AP Photo/picture alliance

Chama kikubwa zaidi cha wafanyakazi nchini Israel, cha Histadrut, kinachowakilisha wafanyakazi 800,000, kimsema leo kuwa kitaitisha mkutano katika siku zijazo kupanga mgomo wa mkubwa wa taifa zima.

Jaji mkuu wa Mahakama ya Juu, Esther Hayut, pamoja na majaji wengine watano wakuu, walikatiza safari ya kwenda Ujerumani ili kushughulikia mzozo huo.

Soma pia:Maandamano dhidi ya serikali yatanda Israel

Msemaji wa mahakama hiyo alisema. Majaji hao walitarajiwa kutua Jumanne usiku, siku moja mapema kuliko ilivyotarajiwa, kujadili mashauri yaliowasilishwa mahakani kupinga marekebisho hayo.

Lakini hatua yoyote yamahakama kubatilisha sheria mpya ya Netanyahu inaweza kusababisha mzozo wa kikatiba na kuwaweka majaji katika mkondo wa mgongano ambao haujawahi kushuhudiwa na serikali ya Israel.