1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madai ya kumshambulia mpenzi yamponza winga wa United

10 Septemba 2023

Manchester United imesema winga Anthony Matheus dos Santos hatorudi katika kikosi cha timu hiyo hadi atakaposhughulikia tuhuma za kumshambulia mpenzi wake.

https://p.dw.com/p/4WARy
UK Manchester | Protest von weiblichen fans gegen Rückkehr von Mason Greenwood
Picha: Female Fans Against Greenwood’s Return

Katika taarifa fupi, United imesema wachezaji ambao hawajashiriki mechi za kimataifa wanatarajiwa kurejea mazoezini Jumatatu. Hata hivyo, wamemekubaliana na Anthony kwamba atachelewa kurejea kikosini hadi atakaposhughulikia tuhuma hizo.

Antony aliondolewa kwenye kikosi cha Brazil katika mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia,wakati kukiwa na uchunguzi wa polisi kuhusu madai ya kumshambulia mpenzi wake wa zamani Gabriela Cavallin.

Soma pia: Mashabiki wa Manchester United wapinga kurejea kwa Mason Greenwood

Hata hivyo Antony amekanusha madai hayo akisema hana kosa lolote. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram mchezaji huyo amesisitiza kuwa hana hatia na atashirikiana kikamilifu na polisi kuwasaidia kupata ukweli, na anatarajia kurudi mchezoni haraka iwezekanavyo.

Wanawake wawili zaidi wamejitokeza kudai walipigwa na Antony, ambaye hajakamatwa wala kufunguliwa mashtaka na amekanusha madai hayo. Polisi wa Brazil na wa Manchester, wanachunguza pia madai hayo.