1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron, Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya ziarani China

5 Aprili 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wameanza ziara ya siku tatu nchini China.

https://p.dw.com/p/4PiVj
Ufaransa | Emmanuel Macron na Ursula von der Leyen mjini Paris
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kulia) na Rais wa Halmamshauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Waliwasili mjini Beijing leo kwa ziara inayonuiwa kuishawishi China kutounga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, wakati pia wakiweka mahusiano ya karibu na mshirika huyo muhimu wa kibiashara.

Akizungumza mjini Beijing, Macron amesema China inaweza kuwa na mchango muhimu katika kupatikana mkondo wa amani nchini Ukraine.

Macron na Von der Leyen watakutana na Rais wa China Xi Jinping pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Katika hotuba yake wiki iliyopita, Von der Leyen aliionya Beijing dhidi ya uungaji mkono wa moja kwa moja vita vya nchini Ukraine, wakati akifuta uwezekano wa Umoja wa Ulaya kujitenga na China.