1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron aanzisha mazungumzo magumu ya serikali mpya Ufaransa

24 Agosti 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameanza duru ya mashauriano magumu na viongozi wa kisiasa, akitumai kuunda muungano unaoweza kutawala baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita ambao haukumpata mshindi wa wazi.

https://p.dw.com/p/4js3l
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Kambi ya Macron ilipoteza hadhi yake ya kuwa kundi kubwa la kisiasa bungeniPicha: Ruffer/Caro/picture alliance

Wiki sita baada ya uchaguzi wa haraka ambao hakuna chama kilichopata wingi wa kutosha wa viti bungeni na ambao kambi ya Macron ilipoteza hadhi yake ya kuwa kundi kubwa la kisiasa, bado hajamtangaza waziri mkuu mpya.

Soma pia: Bunge jipya ya Ufaransa kukutana Alhamisi wiki hii

Jukumu la kwanza kuu la waziri mkuu ajaye litakuwa kuwasilisha bungeni mpango wa bajeti ya mwaka ujao. Chama cha siasa za mrengo wa kushoto cha New Popular Front - NFP -- ambacho kiliibuka kuwa kundi kubwa lakini bila kupata wingi wa viti -- kimesema kinataka mchumi Bibi Lucie Castets mwenye umri wa miaka 37 awe mkuu mpya wa serikali. Lakini upande wa Macron unapendelea kuunda muungano na mrengo wa kulia.