1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaLebanon

Mabishano ya vyama yakwamisha uchaguzi wa rais Lebanon

14 Juni 2023

Mgawanyiko mkali wa chama cha Hezbollah kinachoungwa mkono na Iran na wapinzani umepelekea wabunge kushindwa kumchagua rais mpya kwa mara 12 huko Lebanon

https://p.dw.com/p/4SZf7
Libanon Beirut | Präsidentenwahl gescheitert
Wabunge wa Lebanon wakusanyika kumchagua rais.Picha: Hassan Ammar/dpa/picture alliance

Lebanon imekua haina rais kwa zaidi ya miezi saba, huku jaribio la mwisho la kumchagua rais likiwa limefanyika Januari 19. Kura ya urais kwa wakristo wa madhehebu ya Maronite wa Lebanon ipo chini ya mfumo wa ugawanaji madaraka ambapo chama cha Hezbollah kilimuunga mkono Sleiman Frangieh aliewania kinyang'anyiro dhidi ya Jihad Azour  afisa wa fedha ameidhinishwa na  Wakristo na wabunge huru.

Licha ya kuungwa mkono hakuna hata mmoja aliepata kura za kutosha ili kushinda, Azour amepata kura 59 na Frangieh kura 51 katika bunge lenye idadi ya viti 128. Kinyang'anyiro hicho kinamtaka mshindi kupigiwa kura 65 ili aweze kupita. Wabunge wote walijitokeza kwenye uchaguzi na wengine walitoka nje ya ukumbi baada ya kutumbukiza kura zao kwenye boksi lililopotea baada ya duru ya pili ya uchaguzi. 

Soma Zaidi: Waziri Mkuu Lebanon ajiuzulu

"Makubaliano pekee ndio yataleta mafanikio katika uchaguzi wa urais hatutalazimisha kugombea na wala hatutaruhusu wengine kutulazimishia mgombea" amesema hayo Hassan Fadlallah mbunge wa Hezbollah kabla ya kikao cha Jumatano alipozungumza na waandishi wa habari. Wachambuzi pia wamesema kura hiyo inatishia mkwamo wa kisiasa na kufifisha matumaini ya kuokoa uchumi uliozorota kwa miaka mitatu. "Hatua hii inaweza kuchukua ombwe kwa muda mrefu zaidi" Amesema mchambuzi Krim Bitar.

Libanon Beirut | Präsidentenwahl gescheitert
Spika wa bunge wa Lebanon Nabih Berri akipiga kura.Picha: Hassan Ammar/dpa/picture alliance

Jumuiya ya kimataifa, imewataka wanasiasa kumchagua mgombea urais kwa maridhiano yanayoweza kuisaidia nchi kufanya mageuzi yanayohitajika, na kuwawezesha kupata mikopo ya mabilioni ya dola kutoka nje ya nchi. Lebanon licha ya kutokua na rais, imekua ikitawaliwa na baraza la mawaziri lenye mamlaka yenye mipaka kwa zaidi ya mwaka mmoja, kufuatia muhula uliopita ambapo Hezbollah na washirika wake wamechapisha kwa mara kadhaa kura zilizoharibika ili kuvuruga uchaguzi.

 

Walitumia mbinu kama hiyo katika uchaguzi uliopita, hatua ambayo iliiacha Lebanon bila kuwa na rais kwa takribani miaka miwili mpaka pale Michel Aoun's aliposhinda mwaka 2016. Katika kurasa za mbele za Pro-Hezbollah Al-Akhbar's ziliandika neno moja tu Ombwe. Kwa mujibu wa mkataba wa uongozi uwaziri mkuu ni kwa ajili ya waislam wa sunni na wadhifa wa spika wa bunge ni kwa waislamu wa shia.

Aliekua mbunge wa zamani na waziri Frangieh ambae pia ni rafiki wa rais wa Syria Bashar Al-Assad anatoka katika familia yenye propaganda nyingi kama ilivyo kwa wanasiasa wengi mashuhuri wa Lebanon. Siku ya Jumapili aliahidi atakua "rais wa walebanon wote" licha ya kuwepo muungano wenye mgawanyiko.

Soma Zaidi: Rais wa zamani wa Lebanon akutana na maafisa usalama

 Kufuatia kinyang'anyiro cha urais Azour aliekua waziri wa fedha tangu mwaka 2005 hadi 2008, amejitoa katika nafasi yake ya mkurugenzi wa idara ya Mashariki ya kati na Asia ya kati katika shirika la fedha la kimataifa IMF.

Präsidentschaftskandidaten Jihad Azour und Suleiman Franjieh
Wanaowania nafasi ya Urais Lebanon, Jihad Azour na Suleiman Franjieh.Picha: dpa/picture alliance

Jumatatu alisema anataka kuchangia "suluhu na si migogoro" huku akitangaza adhma yake ya kugombea wadhifa huo. Azour amesema "hatamkaidi yeyote" kama ambavyo Hezbollah inavyomtambulisha kuwa "mgombea mwenye kutatua migogoro".

 Nae mchambuzi Bitar aliiambia shirika la habari la Ufaransa AFP kabla ya uchaguzi kuwa kura ya Jumatano inaweza kuwa kama majaribio 11 ya hapo awali, ama "njia ya kujipima nguvu kisiasa kujua uzito wao wa uchaguzi"  na kuona ni kura ngapi wanaweza kupata. Migogoro inaweza kufungua njia ya mazungumzo ya muda mrefu ambayo hatma yake itafikiwa suluhu na mtu wa tatu. 

Marekani na Ufaransa zimetoa upya wito kwa wabunge wa Lebanon kushirikiana na kumchagua rais mpya msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa Anne-Claire Legendre amewataka wabunge kuichukulia tarehe hiyo kwa uzito na kutopoteza fursa nyingine.