1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MABISHANO JUU YA MALIPO YA FIDIA KWA WALIOTIMULIWA MAKWAO POLAND NA JUU YA ADA ZA MASOMO KATIKA VYUO VIKUU UJERUMANI NDIO MADA KUU ZA WAHARIRI HII LEO:

Ramadhan Ali3 Agosti 2004
https://p.dw.com/p/CHPq

Gazeti la MANNHEIMER MORGEN laandika:

"iIe hatari inayozungumzwa na wengi kutokea kutokana na historia ya pamoja itatokana na nani? Mashtaka kutoka upande wa Poland yanalengwa kwa jumuiya za wale waliotimuliwa maskani mwao nchini Poland. Lakini kuyaeleza mashtaka hayo kuwa yatokana na watu waliojiwinda kulipiza kisasi (kwa kuvamiwa Poland na Ujerumani) hakuna anaesadiki tena leo hii kuwa ni hivyo." hilo lilikuwa MANNHEIMER MORGEN.

Ama gazeti la NÜRNBERGER NARCHRICHTEN linaona tuhuma za mwenyekiti wa Jumuiya ya waliotimuliwa makwao huko Poland, bibi Steinbach hazitokani na nia mbaya:Laandika:

"Kinachoaniwa hapa ni pesa tu.Wanaodai hawajali nani analipa fedha hizo.Bibi Steinbach anapendekeza serikali ya Ujerumani,inaweza kujitwika jukumu la kubeba mzigo huo wa malipo hayo ya fidia.Hujuma alioitoa mwenyekiti huyo kwahivyo, hailengwi kwa kila hali upande wa Poland , bali mwishoe, kwetu sisi walipakodi wa Ujerumani.Kwa kukataa kulipa fidia,Kanzela Schröder,amechukua hatua hiyo kutetea masilahi ya raia ."

Tukiligeukia gazeti la FRANKFURTER NEUE PRESSE,linamkosoa Bibi Steinbach kwa kuandika:

"Ni vigumu sana kuwasadikisha wajerumani kuwa kuna o shina lolote linalopinga wale waliotimuliwa makwao.Lakini nyuma ya madai ya malipo ya fidia yanayolengwa kwa serikali ya Poland au kwa serikali ya Ujerumani, hakuna zaidi ya 10% ya wajerumani waungaomkono.Kwahivyo, hata jumuiya inayowatetea wahanga hao inapaswsa kufunua macho na kutambua ukweli wa hali hiyo ya mambo." hilo lilikua FRANKFURTER NEUE PRESSE.

Msimamo wazi kumuungamkono Kanzela Schröder juu ya mabishano haya, umechukuliwa na gazeti la LANDESZEITUNG kutoka Lüneburg.

Gazeti lachambua :

"Kile Kanzela Schröder kama mfanya-mageuzi anashindwa kukitimiza mara nyingi katika msitu wa siasa za ndani ,amekuwa akifanikiwa katika siasa za nje:Mjini Warsaw, Schröder kwa kujitoa kwake hadharani kwa heshima na utu ,ametoa ishara njema kwa Poland.Kujitoa wazi wazi kwa kizazi cha Ujerumani cha baada ya vita bila kuwa na hisia za hatia kwa yaliotendeka,hakuna maana kutaka kuiandika upya historia.Tangu nchini Poland hata Jamhuri ya Czech, mtu anaelewa vyema kwamb, msimamo wa Jumuiya ya wale waliotimuliwa maskani mwao katika nchi hizo mbili, hauwakilishi wajerumani wengi.Kuwakatalia malipo ya fidia alikofanya Kanzela Schröder , ni sawa na kule kukataa kwa Kanzela Kohl , marekebisho yoyote ya mipaka ya mashariki mwa Ujerumani iliocgorwa baada ya vita."

Gazeti la KÖLNER STADT-ANZEIGER linatugeuzia mada likituchukua katika mjadala wapili motomoto nao ni juu ya ada za masomo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu:gazeti laandika:

"Serikali iunapaswa kuhakikisha kwamba ada za masomo zinatumika kwa mradi uliokusudiwa –yaani fedha hizo zitumike kikamilifu kuigharimia vyuo vikuu.Na hapa ni kudai haki:Ikiwa ada hizo zitageuka kutumiwa kujaza viraka katika mfuko wa hazina za serikali za mikoa,bora ni kuacha kabisa.Ikiwa ada za masomo zitatumika kuboresha haliz ma masomo,hii yaweza kuongoza katika mashindano barabara baina ya vyuo vikuu na kuwanufaisha tangu wanafunzi hata vyuo vikuu vyenyewe."

Likituk kwa jicho la nadharia zozote kushikamanisha na swali hili , si barabara.Laandika kuwa, chama-tawala cha SPD kiinahisi kusoma bure ni matunda yaliovunwa na wanyonge katika hapo kuwastusha wanafunzi wa tabaka la chini la wanyonge kutambua kwamba elimu irudi tena kuwa swali la wale wanaojiweza kifedha ....."