1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Urusi yawakumbuka wahanga wa shambulio la Moscow

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Mabalozi kutoka nchi kadhaa za kigeni wameshiriki hafla ya kuwakumbuka wahanga wa shambulio la mjini Moscow lililofanyika kwenye jumba la tamasha na kusababisha vifo vya makumi ya watu.

https://p.dw.com/p/4eHJB
Moscow 2024 | Urusi
Mabalozi wa baadhi ya nchi za kigeni wakiweka maua katika eneo la kumbukumbu la shambulio la MoscowPicha: Sergei Ilnitsky/AP Photo/picture alliance

Mabalozi kutoka nchi kadhaa za kigeni wameshiriki hafla ya kuwakumbuka wahanga wa shambulio la mjini Moscow lililofanyika kwenye jumba la tamasha na kusababisha vifo vya makumi ya watu. Watu wenye silaha waliwafyatulia risasi watu waliohudhuria tamasha  hilo mnamo Machi 22, katika shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini Urusi katika miongo miwili na kusababisha vifo vya watu takriban 144.

Baadhi ya mabalozi waliohudhuria shughuli ya kuweka maua katika eneo la karibu na ukumbi huo ni kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya, Amerika ya Kusini, Afrika na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengineyo.Macron asema kundi la IS lilitekeleza shambulio la Moscow

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, lilidai kuhusika na shambulio hilo huku maafisa wa Marekani wakisema kwamba wanazo taarifa za kijasusi shambulio hilo lilifanywa na tawi la mtandao wa kundi hilo nchini Afghanistan la Islamic State Khorasan (ISIS-K).