1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano Kenya, watu 7 wakimbizwa hospitalini

27 Juni 2024

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba watu saba wamepelekwa hospitalini katika mji wa Homa Bay magharibi mwa nchi hiyo, kufuatia maandamano ya kitaifa ya kuipinga serikali.

https://p.dw.com/p/4hbFI
Kenya I Maandamano ya kitaifa kupinga muswada wa fedha
Wakenya wamekuwa wakiandamana kushinikiza kutupiliwa nje kwa muswada wa fedha wa mwaka 2024Picha: Tony Karumba/AFP

Licha ya kuahidi kuuondoa muswada wa fedha unaozozaniwa nchini humo, waandamanaji nchini humo wameendelea kuandamana kuipinga serikali ya Rais William Ruto siku ya Alhamisi.

Hali iliripotiwa kuwa ya wasiwasi katika mji mkuu, Nairobi, ambako waandamanaji walitangaza kuelekea ikulu yaliko pia makaazi rasmi ya rais.

Kundi la kwanza la waandamanaji lilikusanyika mchana wa leo katikati mwa jiji la Nairobi ambako maduka mengi yalikuwa yamefungwa.

Picha za televisheni zilionyesha polisi wakitumia gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji huku kukiripotiwa milio ya risasi.