1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfghanistan

Watu 78 wamefariki dunia katika msimu wa baridi

19 Januari 2023

Maafisa wa Taliban wamesema kwamba watu 78 wamefariki dunia katika kipindi cha zaidi ya wiki moja tu wakati wa majira ya baridi nchini Afghanistan, jambo linalouzidisha mgogoro wa kibinadamu nchini humo.

https://p.dw.com/p/4MRdq
BG | Schnee und Eis
Picha: PPI/Zumapress/picture alliance

Msemaji wa Taliban katika wizara ya usimamizi wa majanga Shafiullah Rahimi amesema vifo hivyo vimetokea tangu Januari 10.  Rahimi ameongeza kwamba zaidi ya mifugo 75,000 pia wamefariki kutokana na baridi kali. Amesema utawala wa Taliban umejaribu kuwasaidia zaidi ya watu milioni moja kote nchini humo na bado wanajaribu kuzifikia familia nyingi zaidi kuzisaidia.