1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa Mali, Burkina Faso na Niger wakutana Niamey

Sylvia Mwehozi
19 Agosti 2023

Maafisa wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger wamekutana kujadili mkakati wa pamoja wa kukabiliana na jaribio lolote la uingiliaji kati kijeshi kutoka Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.

https://p.dw.com/p/4VM2O
Niger, Niamey | Mali und Burkina Faso demonstrieren Solidarität mit der Junta von Niger
Picha: RTN/Reuters

Maafisa wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger wamekutana kujadili mkakati wa pamoja wa kukabiliana na jaribio lolote la uingiliaji kati kijeshi kutoka Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS.Niger yavunja makubaliano ya kijeshi na Ufaransa

Televisheni ya taifa ya Niger, imeripoti kwamba maafisa wa kijeshi kutoka nchi hizo tatu wamekutana mjini Niamey, Niger kuamua hatua thabiti endapo ECOWAS itaamua kuchochea vita.

Nchi zote tatu zimekuwa chini ya utawala wa kijeshi tangu kufanyike mapinduzi na hivyo kusimamishwa uanachama ndani ya jumuiya hiyo ya kikanda.

ECOWAS ilitangaza Ijumaa jioni kwamba vikosi vyake viko tayari kuingilia kati Niger, vikisubiri tu amri. Lakini wakati huo huo, duru zinasema ujumbe wa ECOWAS umewasili mjini Niamey leo kwa juhudi za kuanzisha mazungumzo na viongozi wa kijeshi ili kuutatua mzozo huo kwa njia ya demokrasia.