1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Maafisa: Urusi imefanya mashambulizi ya droni mjini Kyiv

31 Julai 2024

Urusi imefanya mashambulizi ya kushtukiza ya kutumia droni kwenye mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na maeneo jirani usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4ivrw
Viunga vya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv.
Viunga vya mji mkuu wa Ukraine, Kyiv. Picha: Vadim Ghirda/AP Photo/picture alliance

Taarifa hizo zimetolewa na uongozi wa kijeshi wa Ukraine kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram.

Kiongozi wa kamandi ya kijeshi ya mji wa Kyiv Serhiy Popko amesema mifumo ya ulinzi wa anga ilifanya kazi ya kuzidungua droni juu ya anga la mji huo.

Mashuhuda waliozungumza na shirika la habari la Reuters wamesema walisikia milio inayooaminikia kuwa ni ya makombora ya mifumo ya ulinzi wa anga yanayotumika kudungua droni au ndege za adui.

Eneo kubwa la mji huo mkuu lilikuwa chini ya hali ya tahadhari ya kutokea mashambulizi ya anga tangu saa mbili usiku jana Jumanne.