1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafa ya wakimbizi kwenye mwambao wa Uitalia:

11 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFkP
ROMA: Waalbania wapatao 21 wamezama katika maafa yaliyowakumba wakimbizi kwenye mwambao wa Uitalia ya Kusini, iliripoti TV ya Uitalia. Polisi wa Kitaliani wameripoti kuwa watoto wawili ni miongoni mwa watu waliofariki. Kuanzia miaka ya 90 watu kwa maelfu wameitumia njia ya bahari kujaribu kuwasili katika mwambao wa Uitalia kutokea maeneo ya Adria.