1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maadhimisho ya mauwaji ya raia wa Kivu mashariki ya Congo

Mitima Delachance1 Oktoba 2021

Mashirika ya kiraia na yale ya haki za binadamu yameadhimisha leo Ijumaa mjini Bukavu,mauwaji ya raia yaliofanywa mnamo kipindi cha miongo miwili huko Kivu.

https://p.dw.com/p/4187I
Demokratische Republik Kongo Süd-Kivu | Banyamulenge Community
Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Siku hii ya maadhimisho imeanza na misa  iliyosomwa ndani ya kanisa la kathedrali malkia wa amani mjini Bukavu napia katika baadhi ya makanisa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kivu kusini  kuombea amani nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Wakati wa misa, Askofu MKuu wa Kanisa katoliki wa mji wa Bukavu François-Xavier Maroyi amesema kuwa siku hii pia ni muda mwafaka kuomba yatekelezwe mapendekezo ya ripoti ya mapping iliyo chapishwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka elfu mbili na kumi (2010), inayoangazia uhalifu na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vilivyofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mnamo mwaka 1993 hadi mnamo mwaka 2010. 

''Inatukumbusha miaka 11 tangu hiyo mapping repoti ya Umoja wa Mataifa itolewe. Yaliotufikia hapa tuyaweke mikoni mwake Mungu,tukimuomba atupatiye maisha mapya'' alisema Askofu Mkuu François-Xavier Maroyi. 

Kati ya wanaoshiriki hafla hii ni hasa wabunge wa mkoa wa kivu kusini na viongozi wa matabaka mbalimbali pamoja na mashirika ya kiraia, wote pamoja wakidai kutendewa haki.

Soma pia: UN: Watu 13,000 waliuawa DRC mnamo miezi minane iliyopita

Mito ya kutendeka kwa sheria Kivu

Daktari Mukwege ameomba kuundwa mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Congo
Daktari Mukwege ameomba kuundwa mahakama ya kimataifa kwa ajili ya CongoPicha: DW/E. Muhero

Kwa mara kadhaa, mshindi wa tuzo ya Nobel mnamo mwaka 2018 Daktari Denis Mukwege ametaka iundwe mahakama maalum ya kimataifa itakayo jihusisha na maovu yaliyo tendeka na yanayoendelea kutendeka hadi sasa nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Emery Mutunzi ni mkaazi wa Bukavu akiwakilisha wakfu wa Panzi wa daktari Denis Mukwege.

''Hiyo mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Congo mabayo tunaomba ni utashi wa viongozi wa kisiasa pamoja na Umoja wa Mataifa kwa sababu ulimwengu ni mmoja kwetu sote.'' alisema  Matunzi.

''Watu wengi hawapendi uhalifu ufahamike''

Wakati wa ushuhuda mbalimbali, wanaharakati wa mashirika ya utetezi wa haki za kibinadamu wamehakikisha kuwa hadi sasa wanazidi kugundua mashimo mengine mlimo zikwa watu tangu zaidi ya miongo miwili na ambayo yangetakiwa ukweli wake ujulikane na adhabu zitolewe. Jean-Moreau Tubibu ni mwanaharakati wa shirika la utetezi wa haki za kibinadamu Groupe Jérémie.

Mauwaji yanaendelea Kivu kwa zaidi ya miongo miwili
Mauwaji yanaendelea Kivu kwa zaidi ya miongo miwiliPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

'' Watu wengi hawapendi uhalifu huo ufahamike. Kuna mauwaji ya raia yaliofanyika huko Kanyola, tumegundua makaburi ya pamoja huko Katogota,huko Shabunda watu walitupwa kwenye mto. Na watu hawafahamu ukweli na hata huko Kaziba kila kitu kimefichwa.'',alisema Tabibu.

Soma pia:Vita visivyokwisha vya makundi ya wanamgambo nchini Congo

Tukio hili linajiri wiki moja baada ya kundi la wabunge waliofanya msafara wakizunguuka katika wilaya za kivu kusini ili kuhamasisha wakaazi kuhusu ripoti ya mapping na namna ya kudai haki mbele ya umoja wa mataifa.