1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBURG. Umoja wa Ulaya wataka amani idumishwe Togo.

29 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIG

Umoja wa nchi za Ulaya umeelezea wasiwasi wake kufuatia vurugu za kisiasa zilizozuka nchini Togo baada ya matokeo ya uchaguzi wa urais siku ya jumapili.

Rais wa Umoja wa Ulaya amezitaka pande zote mbili kuhakikisha hali ya usalama imerejea nchini Togo.

Watu wapatao 22 wameuwawa mwanzoni mwa wiki kufuatia fujo na maandamano baada ya upinzani nchini humo kupinga ushindi wa Faure Gnansigbe katika uchaguzi huo wa urais.

Taasisi ya kijerumani ya Goethe ilitiwa moto baada ya kuvamiwa na watu waliojihami kwa silaha.

Habari kutoka Lome zinasema kuwa hasara inayokadiriwa kufuatia moto huo ni Euro 300,000 pamoja na kuharibiwa kabisa na moto huo maktaba ya taasisi hiyo.

Mjini Berlin serikali ya Ujerumani imemtaka muwakilishi kutoka ubalozi wa Togo kufuatilia swala hilo.