1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG. Ujerumani yakataa kuongeze mchango wake kwa umoja wa Ulaya.

13 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNe

Katika mzozo unaondelea kuhusu ufadhili wa kifedha wa jumuiya ya Ulaya katika siku za usoni, waziri wa fedha wa Ujerumani, Hans Eichel, amesisitiza kwa mara nyengine kwamba serikali ya Berlin haitaongeza kiwango cha fedha inachotoa kwa jumuiya hiyo. Katika mkutano mjini Luxembourg na wanachama wengine wa umoja wa Ulaya, Eichel aliikosoa hali kwamba Ujerumani inachukua nafasi ya 11 katika uchumi wa mataifa ya umoja huo, lakini ni ya tatu kwa kutoa fedha kwa jumuiya hiyo. Eichel amedokezea pia kwamba mwaka huu bajeti ya Ujerumani huenda iwe zaidi ya asilimia tatu, kinyume cha sheria za kuidhibiti thamani ya sarafu ya euro.