1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG : Mazungumzo ya Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya yakwama

3 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVL

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Luxembourg hapo jana ulishindwa kutatuwa kikwazo kinachokwamisha kuanza kwa mazungumzo ya kihistoria na Uturuki ya kujiunga na umoja huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Jack Straw akiwasili kuwa mwenyekiti wa mazungumzo ya siku ya pili baada ya kulala kwa muda mchache amesema hana uhakika iwapo mazungumzo hayo na Uturuki yanaweza kuanza leo hii. Awali alisema mazungumzo hayo ni muhimu na kuelezea kukatishwa tamaa kwake na madai ya Austria kwamba Umoja wa Ulaya ifikirie kuipatia Uturuki ushiriki wa upendeleo maalum badala ya uwanachama kamili wa Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameushutumu Umoja wa Ulaya kwa kutaka kubakia kuwa Klabu ya Wakristo.

Uturuki imetishia kususia mazungumzo ya leo hii iwapo haitopewa uwanachama kamili wa Umoja wa Ulaya.