1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON. Wito watolewa uchunguzi ufanyike tena juu ya kifo cha Jean Charles

19 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjp

Mkuu wa Polisi mjini London anakabiliwa na shinikizo huku mwito ukitolewa wa kufanywa tena kwa uchunguzi juu wa kifo cha Jean Charles de Menezes raia wa Brazil aliyeuwawa kwa kupigwa risasi na polisi mjini London mwezi uliopita.

Ian Blair mkuu wa polisi mjini London amekanusha madai kwamba polisi mjini humo wanafunika ukweli wa kifo cha raia huyo wa Brazil ambae walimuuwa baada kumshuku kuwa mshambuliaji wa kujitoa muhanga.

Raia huyo wa Brazil alipigwa risasi nane kichwani katika kituo cha gari moshi la chini kwa chini.

Kituo kimoja cha televisheni mjini London kilipokea ushahidi wa siri ulio onyesha kuwa marehemu Jean Charles alikuwa amezuiwa na polisi kabla ya kuuwawa na pia hakuonyesha dalili zozote za kuzusha taharuki habari zinazotafautiana na ripoti ya awali iliyo tolewa na polisi.

Mapema wiki ijayo ujumbe kutoka Brazil utawasili nchini Uingereza kuzungumza na wachunguzi.