1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London/Vienna: Marekani yapinga muswada wa Iran Marekani ilisema hiyo ...

19 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFzw
jana, kwamba muswada wa azimio juu ya Iran kutotekeleza wajibu wake wa Kinyuklia hakukubaliki, huku kikundi cha upinzani cha Iran kikiishutumu Tehran juu ya kuficha "mpango wa silaha za atomiki" mbele ya Marekani. Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zilisambaza muswada wa azimio lililokosoa historia ya muda mrefu ya Iran, juu ya kuficha mpango wake wa atomiki, ijadiliwe na wakuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani IAEA hiyo jana. Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Colin Powell alivunjwa moyo na kazi zinazoendeshwa na madola matatu makubwa kabisa katika Umoja wa Ulaya. Hapo awali mjini Brussels, Powell aliishutumu Iran kwenda kinyume na mkataba wa kimataifa dhidi ya silaha za atomiki, akaashiria kwamba azimio lolote lile lazima litambue rasmi ukweli huo.