1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza yatakiwa kuendelea na uidhinishaji wa katiba ya umoja wa Ulaya.

5 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF6k

Uingereza imejibu kwa tahadhari wito uliotolewa na kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder na rais wa Ufaransa Jacques Chirac wa kuendelea na uidhinishaji wa katiba ya Ulaya.

Katiba hiyo ilikataliwa katika kura za maoni zilizofanyika katika nchi mbili na wapiga kura wa Ufaransa na Uholanzi. Msemaji wa serikali ya Uingereza amesema kuwa kunatakiwa kuwa na kipindi cha kufikiria yaliyotokea kwanza kabla ya mkutano wa umoja huo hapo Juni 16.

Vyombo vya habari nchini Uingereza vimesema kuwa waziri wa mambo ya kigeni wa nchi hiyo Jack Straw anaweza kutangaza kuchelewesha kura ya maoni nchini humo ambayo inatarajiwa kufanyika mwaka ujao.

Bwana Schroeder na Chirac walikutana mjini Berlin jana na watakuwa na mazungumzo zaidi mjini Paris mwishoni mwa wiki ijayo. Kamishna wa umoja wa Ulaya kutoka Ireland Charlie McCreevy amesema kuwa watu wengi katika bara la Ulaya wamekasirishwa kwasababu wanaamini kuwa wanasiasa wa Ulaya hawajui tena matatizo ya wananchi wao.

Wakati huo huo wapiga kura wa Uswisi ambayo haimo katika umoja wa Ulaya , wanaelekea kwa kiwango kidogo kuidhinisha kujiunga na eneo la umoja wa Ulaya ambalo halina mipaka na wasafiri wanaingia bila passport, makubaliano yanayojulikana kama Schengen.