1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Uingereza yataka msaada wa Umoja wa Mataifa

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCES

Serikali ya Uingereza imetoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha hati kuitaka Iran iwaachilie huru moja kwa moja wafanyakazi 15 wa jeshi la wanamaji la Uingereza. Wanadiplomasia katika Umoja wa Mataifa wamesema mswada wa hati hiyo umewasilishwa kwa wanachama wengine 14 kwenye Baraza la Usalama ili mswada huo upate kujadiliwa hii leo.Uingereza imelaani pia hatua ya kuonyesha kwenye televisheni ya Iran,kanda ya video ya hao wanamaji waliokamatwa na vikosi vya Iran Ijumaa iliyopita.Iran inasema wanamaji hao wa Kingereza waliingia eneo la Iran, lakini naibu mkuu wa jeshi la wanamaji la Uingereza,Charles Style amewaambia waandishi wa habari mjini London kuwa hatua ya kuwazuia wanamaji hao si halali.Vile vile akaonyesha ramani ambazo amesema hudhihirisha kuwa walipokamatwa,wanamaji hao wa Kingereza walikuwa baharini,umbali wa kama maili mbili kutoka eneo la Iran.