1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza yasikitishwa na kifo cha Mbrazil, lakini sheria ya kuuwa itaendelea.

25 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEqp

Serikali ya Uingereza imesema kuwa inasikitishwa sana na kifo cha Mbrazil ambaye hakuwa na hatia wakati wa msako wa watuhumiwa wa ugaidi, lakini kwamba polisi walilazimika kufanya uamuzi wa ghafla katika tukio ambalo lilihusika na uwezekano wa kitisho cha hatari.

Msemaji wa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair pia amesema waziri wa mambo ya kigeni Jack Straw amezungumza na waziri mwenzake wa Brazil juu ya kifo hicho cha kusikitisha.

Polisi walimpiga risasi na kumuua Jean Charles de Menezes mwenye umri wa miaka ambaye ni fundi umeme katika kituo cha chini ya ardhi cha Stockwell siku ya Ijumaa.

Mkuu wa polisi wa mji wa London Ian Blair amesema kuwa amri hiyo ya kuua bado itatumika.

Wakati huo huo polisi wamemkamata mtu wa tatu anaetuhumiwa kuhusika na jaribio la siku ya Alhamis la kulipua mabomu mjini London.

Msemaji wa polisi amesema kuwa watu hao watatu bado hawajafunguliwa mashtaka.