1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Salam za rambi rambi kwa kifo cha Cook

7 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEnB

Salam za rambi rambi zimekuwa zikitolewa kufuatia kifo cha waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Uingereza Robin Cook ambaye amezirai na kufariki wakati akipanda mlima huko Scotland hapo jana.

Cook amefariki akiwa na umri wa miaka 59.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema Cook alikuwa mwanasiasa mwenye akili ya aina yake,dira na mfasaha wa kusema.Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Philippe Douste-Blazy amesema Cook alikuwa ametopea Uulaya kimtizamo na kwamba aliimarisha mawasiliano kati ya Uingereza na Ufaransa.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Australia Alexander Downer amepongeza juhudi za Cook kuweza kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa kuingilia kati huko Timor ya Mashariki hapo mwaka 1999. Mwaka huo huo Cook pia alikuwa na dhima katika kampeni ya Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO kuwalizimisha wanajeshi wa Serbia kuondoka Kosovo.

Cook alijiuzulu kwenye baraza la mawaziri la Uingereza hapo mwaka 2003 kupinga uamuzi wa Waziri Mkuu Tony Blair kuivamia Iraq.