1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Polisi wamekiuka sheria za afya na usalama

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ae

Polisi wa jiji la London nchini Uingereza wamekutikana na hatia ya kukiuka sheria za afya na usalama na kusababisha kifo cha raia wa Brazil,miaka miwili iliyopita.Jean Charles de Menezes aliekuwa na umri wa miaka 27 kwa makosa alipigwa risasi kichwani na polisi mara saba, baada ya kudhaniwa kuwa ni mshambulizi wa kujitolea muhanga,katika kituo cha treni mjini London.Mahakama imeitoza polisi ya jiji la London faini ya Euro milioni moja na ilipe pia gharama zilizopindukia Euro nusu milioni.