1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Marekani yaitaka Iran itekeleze mapendekezo ya Umoja wa Ulaya

2 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFaK

Marekani imeitaka Iran ifuate mapendekezo ya Umoja wa Ulaya ya kutatua mzozo wa silaha za atomu. Kinyume cha hapo, Iran itafikishwa kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa, alisema waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Condoleeza Rice, alipokuwa akiutembelea mji mkuu wa Uingereza.

Kabla ya hapo, mjumbe w Iran, CIRUS NASSERI, aliiambia taasis ya kimataifa ya nishati ya atom kwamba, nchi yake haiwezi, kuacha kabisa kurutubisha madini ya Uranium, kama vile inavyodaiwa na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya. Alisema, Iran inaweza kuwahakikishia walimwengu kuwa inataka kutumia nishati ya kinyuklia kwa matumizi ya amani peke yake.