1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON. Blair azindua ilani ya kisiasa ya chama cha Labour.

13 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFNY

Waziri wa Uingereza bwana Tony Blair, leo hii amezindua ilani ya kisiasa ya chama chake cha Labour mjini London. Ilani hiyo, inayoitwa Uingereza mbele na wala sio nyuma, inaangazia maswala kama vile uchumi thabiti, afya, elimu na kupambana na uhalifu. Programu hiyo pia inaijumulisha ahadi ya kutoiongeza kodi ya mapato. Kuhusu uhamiaji, swala ambalo limetiliwa mkazo na upinzani, Blair amesema serikali yake ya Labour itaunda sheria kali za kukabiliana na uhamiaji. Waziri Blair anayetarajiwa kushinda awamu ya tatu katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 5 mwezi Mei, anapanga kujiuzulu wakati wa awamu yake ya mwisho madarakani, na nafasi yake kuchukuliwa na waziri wa fedha bwana Gordon Brown.