1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LILONGWE:Rais wa Malawi Bingu Wa Mutharika kuupinga mahakamani mswaada dhidi yake

27 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEzV

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika ameupinga mswaada wa kutaka kumuondoa madarakani na kuutaja usio na msingi.

Rais huyo amesema anapanga kuupinga mswaada huo mahakamani kwa mujibu wa mwanasheria mkuu nchini humo Ralph Kasambara.

Mswaada huo uliwasilishwa bungeni wiki iliyopita na chama cha United Demokratic Front UDF ambacho Wa Mutharika alipata urais kupitia chama hicho lakini sasa rais huyo wa Malawi amekipa kisogo chama hicho na kuunda chama chake binafsi cha Demokratic Progressive Party.

Alhamisi iliyopita bunge lilianza majadiliano juu ya mswaada wa kumuondoa madarakani wa Mutharika lakini majadiliano hayo yalikatizwa baada ya spika wa bunge kuzirai.

Bunge la nchi hiyo limefungwa kwa muda usijulikana.