1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yajadili utaratibu wa kuangamiza silaha.

21 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFqf
VIENNA: Siku moja baada ya kutangaza shabaha yake ya kuteketeza silaha zake za kuangamiza, Libya imeanzisha mjadala pamoja na Shirika la Kimataifa la Kinyuklea - IAEA kuhusu utararibu wa kuangamiza silaha hizo. Shirika la Habari la Austria limearifu, ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Tripolis ulizungumza mjini Vienna pamoja na Mkuu wa Shirika hilo la IAEA, Mohammed El Baradei juu ya miradi ya silaha ya Libya. Baada ya mazungumzo ya kisiri yaliyodumu miezi tisa pamoja na Marekani na Uingereza, hapo Ijumaa ya jana Libya ilitangaza shabaha yake hiyo kwamba itateketeza silaha zake zote za kuangamiza pamoja na kukomesha miradi yake ya kuunda silaha hizo. Serikali kadha za dunia zimekaribisha shabaha hiyo ya Libya. Upande wake Marekani haikutoa bado kauli ya makini iwapo itaondoa haraka vikwazo vyake dhidi ya Libya.