1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya yajadili utaratibu wa kuangamiza silaha.

21 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFqa
VIENNA: Baada ya Libya kutangaza shabaha yake ya kuteketeza silaha zake za kuangamiza, wawakilishi wa serikali wameanzisha mazungumzo ya mwanzo mjini Tripolis pamoja na Shirika la Kimataifa la Kinyuklea - IAEA kuhusu utararibu wa kuangamiza silaha hizo. Mjini Vienna hapo Jumatatu ya kesho Mkuu wa Shirika hilo la IAEA, Mohammed El Baradei anataka kutangaza matokeo kuhusu mashauriano hayo ya mwanzo. Baada ya mazungumzo ya kisiri yaliyodumu miezi tisa pamoja na Marekani na Uingereza, hapo Ijumaa ya juzi Libya ilitangaza shabaha yake hiyo kwamba itateketeza silaha zake zote za kuangamiza pamoja na kukomesha miradi yake ya kuunda silaha hizo. Serikali kadha za dunia zimekaribisha shabaha hiyo ya Libya. Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair na Rais George W. Bush wa Marekani wamesema uamuzi wa Libya ni ishara njema kwa nchi nyingine kama Iran na Korea ya Kaskazini ambazo huenda zitaamua kwa hiyari kufuata mfano wa Libya na kusamehe miradi yao ya kuunda silaha za kinyuklea.