1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yapeleka madakati wa dharura Libya

17 Septemba 2023

Urusi imesema imepeleka madakati wa dharura 35 pamoja na misaada katika eneo la mashariki mwa Libya baada ya taifa hilo kukumbwa na mafuriko makubwa wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4WRSx
Mkazi akiwa amekaa mbele ya nyumba yake katika eneo la Derna lililoathirika vibaya na mafuriko huko Libya, Septemba 15,2023.
Mkazi akiwa amekaa mbele ya nyumba yake katika eneo la Derna lililoathirika vibaya na mafuriko huko Libya, Septemba 15,2023.Picha: Ahmed Gaber/Xinhua/IMAGO

Taarifa ya wizara ya Masuala ya Dharura ya Urusi imesema jana kwamba ndege ya tatu iliyokuwa na madaktari wabobezi imekwishatua Libya ikiwa na karibu watumishi 35 wa wizara hiyo watatoa huduma za afya kwa waathirika.

Tayari Urusi imepeleka hospitali za kuhamishika, zenye vyumba vya upasuaji na huduma za uangalizi maalumu.

Aidha madaktari hao 35 watatoa huduma maalumu za tiba kwa hadi watu 100 kwa siku kwenye maeneo waliko wahanga, imesema wizara hiyo.