1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIBREVILLE: Gbagbo kukutana na De Villepin-

21 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFzG
Rais wa Cote d'Ivoire, Bwana Laurent Gbagbo, anatazamiwa kuwa na mazungumzo na Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Dominique De Villepin jioni hii, katika mji mkuu wa Gabon Libre-Ville. Duru za kidiplomasia katika mji huo zimearifu, lengo la mazungumzo hayo ni kuboresha uhusiano baina ya Ufaransa na koloni lake la zamani, na kujadiliana kuhusu njia za kufufua utekelezaji wa makubaliano ya amani na kugawana madaraka, baina ya serikali ya Rais Laurent Gbagbo na makundi ya waasi, yaliyosainiwa katika mji wa Ufaransa Marcoussis. Wakati huu Ufaransa ina wanajeshi elfu nne, waliopelekwa nchini Cote d''voire kusimamia amani. Rais Laurent Gbagbo pia anatazamiwa kuwa na mazungumzo na Rais wa Mali Amadou Toumani Touré ijumatatu ijayo, katika mji wa kusini mwa Mali wa Sikasso, moakani na Cote d'Ivoire. Baadae Rais Gbagbo atakua na mazungumzo na Rais wa Bourkina Faso Blaise Compaoré, pia katika eneo la mpakani baina ya Cote d'Ivoire na Bourkina Faso.