1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewandowski achaguliwa mshambuliaji bora wa Bundesliga

Sekione Kitojo
20 Julai 2020

Mfungaji bora wa Bundesliga Robert Lewandowski wa mabingwa Bayern Munich amechaguliwa kuwa mchezaji bora mshambuliaji kwa msimu huu na wachezaji wa ligi, katika kura iliyoendeshwa na jarida la mchezo la Kicker.

https://p.dw.com/p/3fbpX
DFB Pokal Bayern vs Frankfurt Jubel Bayern 2:1  Lewandowski
Picha: picture-alliance/Preiss/Witters

Kicker  limesema  leo kuwa raia  huyo wa  Poland Lewandowski  alipata  asilimia 42.6 ya  kura  kutoka wachezaji  wa  ligi ya  kwanza 270  na  kuongoza  dhidi  ya mshambuliaji  wa  Borussia  Dortmund Jadon Sancho aliyepata asilimia  14.1  na  mchezaji  wa  kiungo  wa Bayern Munich Joshua Kimmich.

Werder Bremen - FC Bayern München
Robert Lewandowski (Jezi Nyekundu) akituliza mpira akiwa karibu na mlinzi wa Werder Bremen Theodor GebreselasiPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Meissner

Lewandowski  alipachika  wavuni  mabao 34 na  kuwa  mfungaji bora  wa  Bundesliga kwa  mara ya  tano  katika muda wake  wa kucheza kandanda. Ana  magoli 55  katika  mashindano  yote msimu huu, kiasi ambacho kinaweza  kuwa  bora  zaidi  wakati  Champions League ikianza  tena mwezi  ujao.

Mchezaji wa  kiungo  wa  Birmingham City Jude Bellingham amejiunga  na  Borussia  Dortmund  ya  Ujerumani  kwa  mkataba mrefu, klabu hiyo  ya  Bundesliga  imesema  leo.

Fußball: Bundesliga  Borussia Dortmund - Eintracht Frankfurt
Jadon Sancho wa Borussia Dortmund ameshika nafasi ya piliPicha: Reuters/L. Kuegeler

Vyombo  vya  habari  vya  Uingereza  mapema  mwezi  huu  viliripoti kuwa  Bellingham  mwenye  umri  wa  miaka  17 , ambaye  alikuwa anawaniwa  na  Manchester United, Arsenal  na  Chelsea, ametia saini  kuitumikia  Borussia  Dortmund  kwa  muda  wa  miaka  mitano kwa  kitita  cha  pauni  milioni 26.

Kocha  wa  klabu  ya  Arsenal  London , Mikel Arteta  amesema klabu hiyo  itaweza  kuvutia wachezaji  bora  hata  kama  haitapata  nafasi ya  kucheza  vikombe  vya  Ulaya  msimu  ujao. Arsenal iko  katika nafasi  ya  kumi  katika  Premier League  na  katika  hatari ya kukosa  nafasi  ya  kucheza  ulaya  kwa  mara  ya  kwanza  tangu mwaka 1995-96.

Jude Bellingham | Preston North End vs Birmingham City -
Jude BellinghamPicha: Imago Images/PA Images/M. Rickett

Nayo  klabu  ya  AS Monaco  imemfungisha  mkataba  kocha  wa zamani  wa  Bayern Munich  na  Croatia  Niko  Kovac  kama  kocha mpya  kwa  mkataba  wa  miaka  mitatu kuchukua  nafasi  ya  Robert Moreno  aliyetimuliwa, klabu  hiyo  ya  Ligue 1 imesema  leo. Moreno ambaye  alichukua  nafasi ya Leonardo Jardin mwezi  Desemba, alitimuliwa  mwishoni  mwa  juma.