1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen moto wa kuotea mbali Bundesliga

28 Agosti 2023

Bayer Leverkusen wameendeleza mwanzo wao mwema wa msimu katika Ligi Kuu ya Ujerumani kwa kuvuna ushindi wa 3-0 walipokuwa ugenini wakicheza na Borussia Mönchengladbach Jumapili.

https://p.dw.com/p/4Vev9
kandanda Bundesliga | Borussia Mönchengladbach - Bayer Leverkusen
Mshambuliaji wa Leverkusen Victor Boniface Picha: Federico Gambarini/dpa/picture alliance

Ushindi huu wa Leverkusen unakuja baada ya kuwalaza RB Leipzig 3-2 katika mechi yao ya ufunguzi wa Bundesliga uwanjani Bay Arena.

Mshambuliaji wao mpya Victor Boniface alifunga mabao mawili jana na kusaidia kuunda moja na tayari ni mchezaji anayependwa an mashabiki wa Leverkusen kutokana na cheche anazozionyesha uwanjani.

Vyanzo: Reuters/DPAE