1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leverkusen haitikisiki kileleni mwa Bundesliga

16 Oktoba 2023

Baada ya mapumziko kupisha mechi za kimataifa, ligi kuu ya Ujerumani inarudi dimbani mwishoni mwa wiki hii, huku Bayer Leverkusen ikiendelea kutulia kileleni mwa jedwali kwa jumla ya pointi 19.

https://p.dw.com/p/4XbCv
Europa League | Bayer Leverkusen vs. BK Hacken
Wachezaji wa Bayer Leverkusen wakiseherehekea baoPicha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Mwaka mmoja ndani ya uongozi wake kwa Bayer Leverkusen, kocha Xabi Alonso amevuka matarajio yote kwa kuibadilisha kwa haraka timu hiyo ya Bundesliga kwa kusajili matokeo mazuri kufikia sasa.

Soma pia: Leverkusen kileleni mwa Bundesliga

Tofauti na hali ilivyo kwa kocha Steffen Baumgart na kikosi chake FC Cologne. Katika jumla ya mechi saba ilizocheza msimu huu, FC Cologne imecharazwa mara 6 na kutoka sare mara moja, na ipo katika nafasi ya mwisho kwenye jedwali ikiwa na pointi moja.

Jumamosi hii (21.10:2023) kuna jumla ya mechi sita, Union Berlin itakuwa mwenyeji wa VfB Stuttgart. Freburg itaikaribisha Bochum.

Vinara wa ligi Bayer Leverkusen itakuwa ugenini katika uga wa Volkswagen Arena kuchuana na Wolfsburg huku Eintracht Frankfurt ikitarajai kuchuana na TSG Hoffeinheim.

Timu iliyopanda daraja msimu huu SB Darmstadt 98 itaikaribisha RB Leipzig katika uga wa nyumbani Merck-Stadion am Böllenfalltor.

Katika dimba la MEWA Arena Mainz 05 itakipiga na mabingwa watetezi Bayern Munich.

Jumapili FC Heidenheim 1846 itachuana na FC Augsburg.