1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leipzig yamsajili Seiwald kutoka Salzburg

27 Februari 2023

Timu inayoishikilia nafasi ya nne katika msimamo RB Leipzig imefanya usajili wa mapema. Leipzig imemsaini Nicolas Seiwald kutoka kwa klabu ndugu RB Salzburg kwa ajili ya msimu ujao.

https://p.dw.com/p/4O1uK
SOCCER - UEFA CL, Wolfsburg vs RBS WOLFSBURG,GERMANY,02.NOV.21 - SOCCER - UEFA Champions League, group stage, VfL Wolfsb
Picha: imago images/GEPA pictures

Seiwald ambaye ni mchezaji wa kiungo cha kati anatarajiwa kuichukua nafasi ya Konrad Laimer iwapo ataondoka na kujiunga na Bayern Munich mwishoni mwa msimu kama inavyotarajiwa.

Kocha wa Bayern Julian Nagelsmann amekuwa akimnyatia sana Laimer na ndio maana Leipzig wameamua kuchukua hatua hiyo ya kufanya usajili wa mapema.

Na sasa katika taarifa Leipzig wamethibitisha kwamva Seiwald ambaye ni raia wa Austria na mwenye umri wa miaka 21, alikuwa na kandarasi na Salzburg hadi mwaka 2026 ila atahama msimu huu utakapofika mwisho.