1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Lavrov kukutana na viongozi wa kijeshi wa Sudan

9 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov anatarajiwa leo kukutana mjini Khartoum na watawala wa kijeshi wa Sudan.

https://p.dw.com/p/4NHFL
Südafrika Besuch Außenminister Lawrow Russland
Picha: Phill Magakoe/AFP

Kwa mujibu wa kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Ali al-Sadiq, mazungumzo hayo yanatarajiwa kuangazia zaidi jukumu la Khartoum katika masuala ya nchi jirani zinazokumbwa na migogoro ikiwemo Chad, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ziara ya Lavrov nchini Sudan inajiri wakati wanadiplomasia wakuu wa Marekani na mataifa mengine ya Ulaya wamehitimisha siku mbili za mazungumzo na viongozi wa kijeshi wa Sudan na vikundi vinavyounga mkono demokrasia ili kushinikiza makubaliano ya mwisho ya kuirejesha nchi hiyo katika kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kidemokrasia.