1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lavrov azuru Eritrea

27 Januari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, jana aliwasili nchini Eritrea katika ziara ya siku moja ambayo haikutangazwa kabla.

https://p.dw.com/p/4MmW0
Minister Sergey Lavrov trifft  Esteban Lazo Hernandez
Picha: Russian Foreign Ministry Press Service/AP/picture alliance

Lavrov ambaye yuko katika ziara yake ya pili barani Afrika katika kipindi cha miezi sita, alikutana na Rais Isaias Afwerki.

Waziri wa Habari wa Eritrea, Yemane G. Meskel, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba majadiliano yao yaliangazia mwenendo wa vita vya Ukraine na kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya nishati, madini, teknolojia ya habari, elimu na afya.

Ziara ya Lavrov kwenye bara la Afrika, ambalo limegawika tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, imemfikisha pia Angola, Eswatini na Afrika Kusini.