1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Lavrov akutana na watala wa kijeshi Sudan mjini Khartoum

10 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amekutana na watawala wa kijeshi wa Sudan katika kituo cha mwisho cha ziara yake barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4NK1g
Sudan Besuch Außenminister Russland Lawrow
Picha: Palace Media Office/REUTERS

Lavrov alifanya mazungumzo na Jenerali Abdel Fattah Burhan, mkuu wa Baraza Tawala la Sudan, pamoja na naibu wake Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo anayeongoza kikosi chenye nguvu kinachofahamika kama RSF.

Shirika la habari la Sudan - SUNA limesema bila kutoa maelezo zaidi kuwa mikutano hiyo ililenga katika kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Ziara ya Lavrov barani Afrika ililenga katika kuimarisha mahusiano na kutanua ushawishi katika wakati ambao mataifa ya Magharibi yanataka kuitenga Moscow kwa kuiwekea vikwazo kuhusiana na vita vya Urusi nchini Ukraine.