1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lavrov aionya Ufaransa kuhusiana na kupeleka jeshi Ukraine

5 Juni 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema Urusi itawalenga washauri wowote wa kijeshi wa Ufaransa watakaokwenda Ukraine kulisaidia jeshi la nchi hiyo katika vita vinavyoendelea.

https://p.dw.com/p/4gepO
Türkiye Antalya Forum | Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov, akizungumza katika jopo katika Jukwaa la Diplomasia la Antalya huko Antalya, Uturuki, Machi 1, 2024.Picha: Khalil Hamra/AP Photo/picture alliance

Lavrov ameyasema haya huko Oyo katika Jamhuri ya Kongo katika ziara yake ya Afrika, bara ambalo nchi kadhaa zinaonekana kuegemea upande wa Urusi sasa baada ya kutopiga hatua na kushushwa mabega na mataifa ya Magharibi. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Urusi vile vile amesema kwamba anaunga mkono kufanyika kwa mazungumzo ili kuleta upatanishi baina ya pande zinazozozana nchini Libya. Lavrov ameyasema haya baada ya kufanya mkutano na Rais wa Jamhuri hiyo ya Kongo Denis Sassou Nguessoambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ngazi ya juu kuhusiana na Libya katika umoja wa Afrika. Libya imegawika huku kukiwa na serikali inayotambulika na Umoja wa Mataifa iliyo na makao yake mjini Tripoli na ikiwa inaongozwa na Abdelhamid Dbeibah na serikali hasimu ya mashariki mwa nchi hiyo iliyo chini ya khalifa Haftar ambaye ana mahusiano ya karibu na Urusi.