1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Laura Lindemann aipatia Ujerumani medali ya dhahabu

5 Agosti 2024

Laura Lindemann ameipatia Ujerumani medali ya dhahabu baada ya kushinda katika mashindano ya Olimpiki ya triathlon yanayohusisha michezo ya kuogelea, kukimbia na kuendesha baiskeli.

https://p.dw.com/p/4j7Ri
Olimpiki Paris 2024 - Triathlon
Laura Lindemann aliposhinda na kuipatia Ujerumani medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki mjini Paris.Picha: Marijan Murat/dpa/picture alliance

Katika mashindano hayo, Marekani ilishikilia nafasi ya pili na kuchukua medali ya fedha, wakati Uingereza ilikamata nafasi ya tatu na kuridhika na medali ya shaba.

Mashindano hayo ya triathlon hata hivyo yaligubikwa na wasiwasi juu ya ubora wa maji katika mto Seine, hali iliyosababisha mbio za wanaume kuahirishwa kwa siku moja.

Soma zaidi: Olimpiki Paris 2024: Wanariadha wa Afrika wang´ara

Hiyo ni medali ya tatu kwa Ujerumani kuwahi kushinda katika mashindano ya Olimpiki ya triathlon.

Jan Frodeno alishinda medali ya dhahabu mjini Beijing mwaka 2008 na Stephan Vuckovic alishinda medali ya fedha mjini Sydney miaka minane iliyopita.