1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LARNACA:Mkutano juu ya Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya

1 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEfM

Mawaziri wa nchi za nje wa Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Newport,huko Welsh Uingereza kujiandaa kwa mazungumzo juu ya pendekezo la Uturuki la kujiunga na Umoja huo.

Mazungumzo ya uwanachama wa Uturuki yanapaswa kuanza oktoba 3 mwaka huu.

Cyprus imetishia kuzuia majadiliano hayo kufuatia mzozo wa kibalozi.

Uturuki imekataa kuitambua serikali ya Cyprus ya wagiriki kusini mwa kisiwa hicho licha ya eneo hilo kuwakilisha kisiwa kizima cha Cyprus katika umoja wa Ulaya.

Badala yake Uturuki ina mawasiliano na eneo la Kaskazini la Cyprus lenye wakaazi wa asili ya kituruki.

Halmashauri ya Ulaya inazidi kuishinikiza Uturuki kufungua bandari zake kwa meli za Cyprus kama sehemu ya umoja wa forodha na nchi zote 25 wanachama wa umoja wa Ulaya.

Kutekelezwa kwa mapatano hayo ni sharti mojawapo la Umoja wa Ulaya ili kufanya mazungumzo na Uturuki.