1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LARNACA: Cyprus kuzuia majadiliano ya Umoja wa Ulaya na Uturuki

1 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEfa

Cyprus imetishia kuweka vizingiti dhidi ya majadiliano yanayohusika na uanachama wa Uturuki katika Umoja wa Ulaya,kwa sababu ya ugomvi wa kibalozi.Kwa hivi sasa,serikali ya Cyprus yenye asili ya Kigiriki kusini mwa kisiwa hicho, haitambuliwi na Uturuki,ingawa eneo hilo huwakilisha kisiwa kizima cha Cyprus katika Umoja wa Ulaya.Badala yake,Uturuki ina mawasiliano na eneo la kaskazini la Cyprus lenye wakaazi wenye asili ya Kituruki.Halmashauri ya Ulaya imezidi kuishinikiza Uturuki kuwa iruhusu meli za Cyprus katika bandari zake,kama sehemu ya umoja wa forodha na wanachama wote 25 wa Umoja wa Ulaya.Kutekelezwa kwa protokoli hiyo ni sharti mojawapo la Umoja wa Ulaya kufanya majadiliano na Uturuki.Majadiliano hayo yanatazamiwa kuanza tarehe 3 Oktoba.