1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Larijan mjini Vienna kwa mazungumzo pamoja na Javier Solana

9 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDy
Mjumbe wa Iran katika mazungumzo ya kinuklea Ali Larijani,yuko Vienna kwa mazungumzo pamoja na muakilishi mkuu wa siasa ya nje ya Umoja wa ulaya Javier Solana.Mkutano huo umesadif wakati ambapo Marekani inapigania azimio la baraza la usalama liiwekee vikwazo Iran kwaajili ya miradi yake ya kinuklea.Mswaada wa azimio hilo utaratibiwa mapema wiki ijayo.Muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa ulaya Javier Solana ameondowa uwezekano wa kuwekewa vikwazo Iran katika wakati ambapo mazungumzo yanaendelea.