1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTaiwan

Lai Ching-te asema yuko tayari kufanya kazi na China

26 Mei 2024

Rais mpya wa Taiwan Lai Ching-te amesema leo kuwa yuko tayari kufanya kazi na China licha ya mapema wiki hii Beijing kufanya luteka za kijeshi karibu na kisiwa hicho chenye utawala wa ndani.

https://p.dw.com/p/4gI8x
Rais wa Taiwan Lai Ching-te akitoa hotuba wakati wa ziara katika kambi ya jeshi mjini Taoyuan
Rais wa Taiwan Lai Ching-te akitoa hotuba wakati wa ziara katika kambi ya jeshi mjini TaoyuanPicha: Ann Wang/REUTERS

Lai amewaambia waandishí wa habari mjini Taipei kuwa anataka Taiwan na China "kubeba kwa pamoja jukumu la kuhakikisha utulivu wa kikanda."

Kiongozi huyo ameendelea kueleza kuwa, anapania kuimarisha maelewano na ushirikiano na China kuelekea kupatikana kwa amani na ustawi wa pamoja.

Soma pia: Luteka za jeshi la China karibu na Taiwan zimemalizika

Mnamo siku ya Alhamisi, China ilifanya luteka za kijeshi katika eneo linaloizunguka Taiwan, siku tatu tu baada ya Lai Ching-te kuapishwa, luteka hizo zikichukuliwa kama kampeni inayoongezeka ya vitisho kwa Taiwan, ambayo China inakiona kisiwa hicho kama sehemu ya himaya yake.

Wakati wa luteka hizo za kijeshi, China iliapa kuwa "vikosi huru" vitaachwa huku vichwa vyao vimevunjika na damu inamwagika."