1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lagos. Wanajeshi wa Nigeria kwenda Dafur kulinda amani katika jeshi la umoja wa Afrika.

30 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEyf

Kundi la kwanza la wanajeshi 2000 wa Nigeria linatarajiwa kuondoka kwenda katika jimbo la Sudan la Dafur kesho Ijumaa kuimarisha jeshi la umoja wa Afrika linalosimamia usitishaji wa mapigano katika eneo hilo.

Mkurugenzi wa habari wa jeshi la Nigeria , brigadia jenerali Ganiyu Adewale amesema kuwa vikosi vitatu vyenye wanajeshi 700 kila kimoja vitachukua nafasi ya wanajeshi karibu 500 wa Nigeria ambao wako katika jimbo la Dafur tangu mwaka 2004.

Kundi la pili la wanajeshi hao litaondoka wiki ijayo, wakati kikosi kingine kitaondoka mwezi wa August.

Jeshi la umoja wa Afrika lenye wanajeshi zaidi ya 2 300 pamoja na mamia ya polisi wa kawaida wako katika jimbo la Dafur wakiangalia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwaka uliopita kati ya waasi ambao wengi wao si Waarabu na serikali ambayo inaendeshwa na Waarabu mjini Khartoum.